Itakumbukwa Mnamo Disemba 5, mwaka huu 2025 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt, Mwigulu Nchemba alifanya ziara jijiji Mwanza kuzitembelea familia zilizopata madhara ya vurugu za uchaguzi Oct 29 pamoja na kuzungumza na wakazi wa jiji hili la miamba.
Pia alipokea kero sugu ya kutokamilika kwa barabara na madaraja kadhaa likiwemo lile la eneo sugu la Mkuyuni.
Katika sehemu ya majibu yake Mhe. Waziri mkuu alitoa agizo kwa Waziri wa Ujenzi kuja na kulikagua daraja hilo haraka iwezekanavyo na kutoka na suluhisho.
Aidha Ujenzi wa Daraja la Mabatini Kuimarisha Usalama na Kupunguza Mafuriko Mwanza
Upanuzi na ujenzi wa Daraja la Mabatini jijini Mwanza haujalenga tu kupunguza msongamano wa magari, bali pia kutatua changamoto kubwa ya mafuriko ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara, hasa yale ya mwaka 2021 na 2024 ambayo yalisababisha madhara makubwa kwa wananchi.
Mradi huu muhimu unatekelezwa chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia kwa gharama ya Shilingi bilioni 6, milioni 300 na 565 elfu.
Awali, ujenzi huo ulikuwa ukamilike tarehe 15 Novemba 2025, lakini kutokana na ucheleweshaji uliosababishwa na kazi ya kuondoa miundombinu ya maji, umeme na mawasiliano, kazi ambayo haikuwa rahisi wala nyepesi.
Mradi huo ulioanza 2024 mkandarasi ameongezewa muda wa siku 45 ambapo sasa mradi unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Desemba 2025.
Mpaka sasa maendeleo ya ujenzi yamefikia asilimia 93, ambapo kazi kubwa iliyosalia ni ujenzi wa kingo za barabara.
Mradi unatekelezwa kwa usimamizi wa TANROADS, huku mkandarasi mkuu akiwa ni NYANZA Roads Works.
Mradi huu unatarajiwa kuleta unafuu mkubwa kwa wakazi wa jiji la Mwanza kwa kupunguza hatari za mafuriko na kurahisisha usafiri katika eneo la Mabatini.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime