Nyota wa soka wa Ufaransa, Kylian Mbappé, ameandika historia mpya ndani ya klabu ya Real Madrid baada ya kufikia rekodi ya muda mrefu iliyowekwa na Cristiano Ronaldo mwaka 2013.
Ambapo Mbappé alifikia rekodi hiyo baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa Real Madrid wa mabao 2-0 dhidi ya Sevilla na kufikisha jumla ya magoli 59 ndani ya mwaka 2025 ambayo ni idadi sawa na ile ya Ronaldo iliyodumu kwa takribani miaka 12.
Hivyo rekodi hiyo ya Ronaldo iliwekwa mwaka 2013 alipokuwa akikipiga ndani ya Real Madrid ambapo alifunga magoli 59 katika michezo 50 huku akitoa pasi za mabao 14.
Kwa upande wake, Mbappé ameonyesha ubora mkubwa msimu huu baada ya kucheza michezo 59, kufunga magoli 59 na kutoa pasi za mabao 6, akithibitisha thamani yake kama mmoja wa washambuliaji hatari zaidi duniani kwa sasa.
Hata hivyo mafanikio hayo yanaifanya historia ya Mbappé kuendelea kuandikwa ndani ya Santiago Bernabéu, huku mashabiki wakianza kumlinganisha moja kwa moja na gwiji wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime