Droo kombe la dunia 2026 kufanyika leo Desemba 05

Droo ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA litakalochezwa mwakani huko Marekani Canada na Mexico itafanyika leo katika Kituo cha Sanaa cha Kennedy huko mjini Washington. 

Ambapo rais wa Marekani Donald Trump na  mwenzake wa Mexico Claudi Sheinbaum pamoja na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney watahudhuria droo hiyo pamoja na Rais wa FIFA Gianni Infantino hivyo timu 11 bora duniani kulingana na orodha ya FIFA zimefuzu mashindano hayo.

Aidha Miongoni mwa timu 48 zitakazoshiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo ya dunia ni Cape Verde, Curacao, Jordan na Uzbekistan.

Hata hivyo Bara la Afrika litawakilishwa na Morocco, Tunisia, Misri, Algeria, Ghana, Senegal, Afrika Kusini, Cape Verde na Ivory Coast.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii