Mkutano wa kilele baina ya AU na EU waanza mjini Brussels

Viongozi wa Umoja wa Afrika na wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kwa mazungumzo ya siku mbili kuanzia leo, wakiazimia kuimarisha ushirikiano, huku Ulaya ikiahidi uwekezaji mkubwa barani Afrika inakokabiliwa na ushindani wa China na Urusi. Akizungumza katika mkutano huo, mkuu wa diplomasia wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel amesema Ulaya inapaswa kuisaidia Afrika kuyashughulikia matatizo yake.Uhusiano baina ya mabara hayo mawili umekuwa ukitiwa doa na mlolongo wa matatizo, yakiwemo usambazaji wa chanjo ya Covid-19, namna ya kuzuia uhamiaji haramu, wimbi la mapinduzi ya kijeshi barani Afrika, na ushawishi wa mamluki wa Urusi barani humo. Rais wa Senegal Macky Sall ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amesema lengo la mkutano huu ni kufikia uhusiano mpya unaodhihirika kwa vitendo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii