WHO kupoteza robo ya wafanyakazi wake ifikapo katikati 2026

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema idadi ya wafanyakazi wake itapungua kwa takriban robo zaidi ya ajira 2,000 kufikia katikati ya mwaka ujao.

Hayo ni katika wakati likijaribu kutekeleza mageuzi baada ya mfadhili wake mkuu, Marekani, kutangaza kujiondoa.Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo kwa nchi wanachama sababu za hali hiyo ni pamoja na kustaafu na kuhama kwa baadhi ya watumishi.

Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trumpulijiondoa kwenye shirika hilo mara tu baada ya kuingia madarakani mwezi Januari, jambo lililosababisha shirika hilo kupunguza shughuli zake na kupunguza timu ya uratibu wake kwa nusu.

Washington ni mfadhili mkubwa zaidi wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, likichangia takriban asilimia 18 ya ufadhili wake wote.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii