TotalEnergies yatuhumiwa kuhusika na vitendo vya uhalifu wa kivita Msumbiji

Shirika la kimataifa la Human Rights Watch, limechapisha taarifa inayoituhumu kampuni ya mafuta ya Ufaransa, TotalEnergies kuhusika na vitendo vya uhalifu wa kivita kwa kushirikiana na askari wanaotoa ulinzi kwenye visima vyake vya gesi nchini Msumbiji.

Kulingana na malalamishi yaliowasilishwa na waendesha mashtaka nchini Ufaransa, TotalEnergies inatuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita, Tuhuma ambazo kampuni hiyo imekanusha.

Kampuni hiyo imekuwa ikikataa kuwajibikia vitendo vya wanajeshi wa serikali ya Msumbiji na walinda usalama wengine waliopewa jukumu la kutoa ulinzi katika kituo chake cha gesi cha Afungi.

Wanajeshi wa Msumbiji waliripotiwa kutekeleza mauaji ya halaiki ya watu katika eneo lenye utajiri wa madini la Cabo Delgado kaskazini mwa nchi hiyo, eneo ambalo wanajeshi wa serikali walikuwa wakipambana na makundi ya kijihadi.

Mwezi Machi mwaka wa 2021, wanajihadi walivamia mji wa Palma ambapo walitekeleza mauaji pamoja na kuwateka raia 1,563 karibu na mradi wa gesi wa kampundi ya  TotalEnergies kwenye eneo la Afungi na kuilazimisha kusitisha kwa muda shughuli zake.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii