Wanafunzi wa muhula wa kwanza watakiwa kuwa Wazalendo na nchi yao

Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Assed Mwampamba Novemba 17 mwaka huu ametoa elimu kwa wanafunzi wa muhula wa kwanza ambao wanajiunga katika Chuo cha Mgao Health Training Institute na kuwataka kuwa wazelendo kwa Taifa na kuacha tabia ya kujiingiza katika makundi ya uhalifu ambayo yamekuwa yakifanya matendo maovu na kinyume na maadili.

Pia, amewataka kuwa na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na kuacha kutumika kama vyanzo vya uchochozi au uhalibifu wa amani nchi bali wazingatie masomo ili kufikia malengo yao ya kitaaluma.

Kwa upande wake, Mkuu dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Njombe Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Oscar Kitaly amewataka wanafunzi hao kuripoti matukio yoyote ya ukatili wa kijinsia bila kuogapa au kuficha ili hatua zichukuliwe ndio maana Kuna "Kampeni ya Tuwaambia kabla hawajaaribiwa" ili wanafunzi wapate uelewa wa masuala ya ukatili na kuchukua hatua.

Sambamba na hilo, amewaasa kuzingatia masomo na kuacha kujihusisha na makundi mabaya ya uhalifu kama Vile ya madawa ya kulevya ambapo mwisho wake unaweza ukafungwa au kupoteza matarajio yako kama mwanafunzi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii