Viongozi watakiwa kuhakikisha wanatafuta zaidi fedha ili kutekeleza miradi ya maendeleo Nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza viongozi kuhakikisha wanatafuta zaidi fedha za ndani ili kutekeleza miradi ya maendeleo Nchin.

Akizungumza Ikulu Chamwino, jijini Dodoma mara baada ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, Rais Samia amesema hali iliyojitokeza nchini wakati wa uchaguzi mkuu imeitia doa nchi na huenda ikapunguza sifa ya Tanzania kupata mikopo kwa urahisi kutoka nje.

Kutokana na hilo, amewataka viongozi kuongeza juhudi za kutafuta fedha za ndani na kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kama ilivyopangwa.

Aidha, Rais Samia alisisitiza kuwa ahadi alizowapa wananchi ni nyingi, huku muda wa utekelezaji ukiwa mchache, hivyo viongozi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, usiku na mchana ili kuhakikisha wanatimiza ahadi hizo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii