Jukwaa la wadau wa mazingira kanda ya Ziwa Victoria watoa elimu matumizi ya taka plastic

Jukwaa la wadau wa mazingira kanda ya Ziwa Victoria chini ya kauli mbiu isemayo"Sema hapana kwa taka za plastic kuwa sehemu ya suluhisho chukua hatua sasa" limeendelea kuwanufaisha wadau mbalimbali hapa nchini kuhusiana na mitazamo ya watu juu ya ukusanyaji na utupaji ovyo wa taka plastic. 

Wamesema hayo leo Novemba 18 mwaka huu katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza kwenye hafla ya ufunguzi wa kampeni ya miaka mitatu ya kutokomeza taka plastic kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii pamoja na wachakataji ili kuongeza majukwaa ya bidhaa zitokanazo na takataka.

Kwa upande wake Elida Edward ambaye ni meneja wa usalama na mazingira Nyanza bolting coca-cola mkoani humo ameeleza kuwa wao kama wazalishaji wa taka plastic wameunda mifumo bora ya kuhifadhia taka sambamba na sehemu za kuchomea taka hizo hivyo amevitaka vikundi vinavyokusanya taka kuangalia namna bora ya kutokomeza taka hizo.

Aidha Batuli Seif afisa maendeleo ya jamii bodi ya maji bonde la ziwa Victoria amefafanua kuwa chanzo cha maji ni sehemu ambako kila mtu hupata huduma ya maji hivyo jamii inatakiwa kuvitunza na kuvihifadhi ili kusaidia kupunguza ongezeko la utupaji taka ovyo na usimamizi rasilimali za serikali kupitia vyonzo vya maji.

Hata hivyo Phinias.B Marcon afisa mazingira wilaya ya Ilemela amewataka vijana kuacha tabia ya kuharibu miundombinu ya kuhifadhia taka plastic zilizowekwa maeneo ya barabara pia kuacha kutupa taka ovyo kutokana na janga la mabadiliko ya tabia ya nchi jambo litakalosaidia kuepukana na magonjwa ya milipuko. 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii