RC Chalamila atangaza rasmi kurejeshwa hudama ya mwendokasi

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert John Chalamila ametangaza rasmi kuwa huduma ya mwendokasi kwa barabara ya BRT 2 (Mbagala) itaanza kufanya kazi rasmi siku ya tarehe 20/11/2025 siku ya Alhamisi na usafiri huo utaanza kuanzia majira ya saa 12 asubuhi hadi saa 2:00 usiku.

Kufuatia malalamiko na tabu wanayopitia wananchi watumiaji wa huduma hiyo ya mwendokasi Serikali imeamua kuwasikiliza na kuwarejeshea huduma hiyo.

Mkuu wa Mkoa amegusia kuwa barabara ya BRT 1 ambayo ni njia ya Kimara bado wanaendelea na tathimini juu ya uharibifu uliofanyika na kuahidi kuwa huduma hiyo itarejeshwa hivi karibuni kwa barabara hiyo ya BRT 1 (Kimara)

Pia Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe. Sixtus Mapunda leo Mara baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert John Chalamila ametoa dukuduku la wakazi wa Temeke juu ya kukosekana kwa huduma ya mwendokasi ambayo mradi huo ulisitishwa mara baada ya machafuko na magari baadhi kuharibiwa pamoja na vituo.

Mhe Sixtus Mapunda ameiomba Serikali kuwasilikiliza wakazi hao wa Temeke na kudai kuwa wao hawana shida wala tatizo na miradi ya Serikali.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii