Rais wa zamani nchini Malawi, Lazarus Chakwera amesema ameridhia uteuzi wa Jumuiya ya Madola kuwa msuluhishi Tanzania.
Chakwera amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama chake MCP mjini Lilongwe nchini humo hapo jana.
Alisema amemjulisha Katibu Mkuu wa Jumuia ya Madola kuhusu kukubali uteuzi, serikali ya Tanzania ikimkaribisha kuwa sehemu ya mazungumzo kama jirani na rafiki, anayesimamia uhamasishaji wa amani ya nchi hiyo na kila nchi katika ukanda.
''Kwa hivyo, timu ya wataalamu kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola jijini London inawasili Dar es Salaam ili kuhakikisha utayari wa serikali ya Tanzania kwa ziara yangu iliyopendekezwa kwa ajili ya mazungumzo kuhusu hali nyeti iliyojitokeza huko na namna ya kuitatua kwa amani'' Alisema Chakwera.
Dkt Chakwera atakuwa Tanzania kwa ziara ya siku nne kuanzia tarehe 18 hadi 21 Novemba, ikiwa ni hatua ya mwanzo ya majadiliano na wadau mbalimbali kuhusu masuala yanayohusiana na uchaguzi na mustakabali wa maendeleo ya nchi.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime