Merz, Macron, Starmer kukutana Berlin leo hii

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz atakutana na viongozi wa Ufaransa na Uingereza mjini Berlin jioni ya leo. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa serikali.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakuwa Berlin mapema kuhudhuria mkutano kuhusu uhuru wa kidijitali barani Ulaya. 

Baada ya mkutano huo, Merz na Macron wataungana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer kwa chakula cha jioni, ingawa mada ya mazungumzo haijafichuliwa.

Mkutano wa uhuru wa kidijitali unalenga kujibu wito wa Ulaya kudhibiti mustakabali wake wa kidijitali, hasa ikizingatiwa nafasi inayoongezeka ya akili bandia (AI) katika sekta mbalimbali. 

Mkutano huo pia utahudhuriwa na wakuu wa kampuni kubwa za Ulaya, ikiwemo kampuni ya AI ya Ufaransa Mistral na kampuni ya programu ya Ujerumani SAP.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii