Upinzani waituhumu serikali ya kijeshi kwa kushindwa kulinda nchi

Mrengo wa upinzani nchini Mali, umeituhumu utawala wa kijeshi kwa kushindwa kuilinda nchi hiyo dhidi  mashambulio ya wanajihadi ambao umesababisha uhaba wa mafuta.

Kwa miezi miwili sasa, jiji kuu la Bamako limeshuhudia uhaba mkubwa wa mafuta na bidhaa za petroli baada ya wanajihadi wa JNIM kuzidisha mashambulio,kufunga barabara na kuzuia usafirishaji wa mafuta pia utekaji wa raia haswa wageni.

Upinzani sasa,umeukosoa utawala wa kiongozi wa kijeshi Jenerali Assimi Goita kwa kushindwa kuipa nchi hiyo ulinzi hali ambayo imeendelea kuathiri shughuli za kiuchumi na kijamii nchini humo.

Hivi majuzi vyuo vikuu na shule zilirejelewa baada ya kufungwa kwa majuma mawili kutokana na usalama mdogo na ukosefu wa mafuta ulioathiri shughuli za kawaida

Hii inajiri huku wizara ya mambo ya nje ikipuzilia mbali madai ya jiji kuu kufungiwa.

Mataifa mengi yamekuwa yakiwashauri raia wao kuondoka Mali kwa hofu kuwa tishio hilo la kigaidi linazidi kuwa kubwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii