Mke wa Besigye atoa wito kuachiwa huru kwa mumewe

Mke wa mwanasiasa mashuhuri nchini Uganda, Kizza Besigye, Winnie Byanyima, sasa anataka mume wake kuachiwa huru na haki itendeke, kauli anayotia wakati huu mwanasiasa huyo akifikisha mwaka mmoja kizuizini tangu alipotekwa nyara nchini Kenya na kurejeshwa nchini mwake.

Baada ya kutekwa jijini Nairobi akiwa na mshirika wake Hajj Lutale, wawili hao walifikishwa katika mahakama ya kijeshi jijini Kampala tarehe 20 mwezi Novemba na kustakiwa kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume na sheria.

Katika taarifa yake, Byanyima amesema kuendelea kuzuiliwa kwa kwa Besigye kunamnyima haki.

Byanyima akiishutumu serikali ya Uganda kwa kumshikilia mumewe kinyume na sheria, kuisikiliza kesi yake katika mahakama ya kijeshi pamoja na kumnyima dhamana.

Kulingana na Winnie, kesi ya Besigye haijawahi kupiga hatua mahakamani ikiwa ni mwaka mmoja sasa tangu azuiliwe kitendo anachosema ni ukiukaji wa haki za mshtakiwa.

Mwezi Januari mwaka huu, mahakama ya kijeshi iliagiza kuwa Besigye anaweza kushtakiwa kwa uhaini.

#Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii