Leopards ya Congo yazima matumaini ya Nigeria kufuzu kombe la dunia

Timu ya taifa ya DRC hapo jana iliweka hai matumaini yake ya kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia hapo mwakani baada ya kuwafunga Nigeria kwa magoli 4 kwa 3 kwa njia ya Penalti baada dakika 90 kutoka sare ya goli 1 kwa 1.

Ushindi huu wa DRC unamaanisha kuwa imekata tiketi ya kuchezaja hatua ya mtoano ya mabara kwa ukanda wa Afrika huko Morocoo na sasa inasubiri kuchezeshwa kwa Droo mwezi Machi ambapo timu 6 zitachuana kutafuta washindi wawili watakaokamilisha timu 48

Mechi za mtoano huko Rabati, Morocoo zilikuwa ni kwa timu zilizomaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi 9 ya ukanda wa Afrika ambapo mechi za awali zilimalizika mwezi uliopita na kupata tiketi ya moja kwa moja.

Egypt, SenegalAfrika KusiniGhanaCape VerdeMorocco, Ivory Coast, Algeria and Tunisia zenyewe tayari zimeshafuzu kwa fainali za mwaka 2026 kutoka Afrika.

Nchi ya Bolivia kutoka ukanda wa Amerika Kusini Pamoja na New Caledonia kutoka ukanda wa Oceania pia zimepata tiketi ya kufuzu katika michuano ya timu 6 hatua ya mtoano, ambapo kutajumuisha pia timu kutoka Falme za Kiarabu au IraqAmerika Kaskazini, Kati na Carribean ambapo timu mbili zitafuzu kucheza fainali za kombe la dunia.

#Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii