ACT-Wazalendo yatoa hoja tatu wanazohiji zitekelezwa

Chama Cha ACT-Wazalendo kimetoa hoja tatu wanazotaka zitekelezwa baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais wabunge na madiwani na mgombea Urais kupitia CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 98 ya kura zote zilizopigwa.

Mojawapo ya hoja hizo ni kuundwe kwa Tume ya Maridhiano iliyo huru itakayoleta pamoja serikali, viongozi wa upinzani na wananchi kwa lengo la kukomesha uonevu na kuweka mfumo bora wa uendeshaji wa nchi.

Ingawa kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati baadhi ya waliokuwa wagombea ubunge wa chama hicho kueleza kadhia walizokutana nazo wakati wa mchakato wa uchaguzi huo.

Aidha hoja nyingine aliitaja ni kutaka kuundwa kwa Tume Huru ya Uchunguzi nje ya serikali ambayo itachunguza matukio yote yaliyosababisha kuvurugwa kwa uchaguzi na watakaobainika walihusika kuuharibu kwa makusudi wawajibike.

Hata hivyo Dorothy alitaja hoja ya tatu ni kufanyike kwa mageuzi ya kidemokrasia hususani Katiba mpya itakayounda Tume Huru ya Uchaguzi, itakayoweka wazi mipaka iliyowazi kati ya dola na chama tawala na kuweka uhuru wa vyombo vya habari na vyama vya siasa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii