Kiongozi wa Kijeshi Aapishwa Kuwa Rais

KIONGOZI wa Kijeshi wa Burkina Faso, Luteni Kanali Paul-Henri Damiba, ameapishwa kuwa rais wa mpito wa taifa hilo.

Akiwa amevaa sare za kijeshi, Damiba ameapa kuheshimu katiba katika hafla ndogo iliyofanyika katika mji Mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Mkuu huyo wa jeshi, ameongoza harakati za mapinduzi yaliyofanyika nchini humo kumuondoa Rais Roch Kaboré madarakani, mwezi uliopita.

Jeshi linasema litarejesha utulivu wa kikatiba lakini halijatoa ratiba ya kurejea utawala wa kiraia.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii