Prof. Msoffe amefanya mazungumzo na Mkuu wa Kitengo cha Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Peter Msoffe amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kitengo cha Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) Bi. Mirey Atallah.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 30 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP30) uliofanyika katika Jiji la Belém, Brazil.

Prof. Msoffe amemueleza Mkurugenzi huyo kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na UNEP katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuimarisha mifumo ikolojia ili kuleta uwiano wa viumbe hai na mazingira.

Alisema Tanzania imejaaliwa kuwa na vyanzo vingi vya maji vikiwemo mito, maziwa na bahari ambavyo ni muhimu katika uhai wa mwanadamu na kwa hiyo Serikali inaishirikisha jamii katika kuvitunza.

Naibu Katibu Mkuu alieleza kuwa kutokana na uwepo wa vyanzo hivyo vya maji, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kuratibu Sekta ya Uchumi wa Buluu ambao tayari Sera yake ilishazinduliwa na 

Akiendelea na mazungumzo hayo, Prof. Msoffe alimueleza mkurugenzi huyo kuwa urejelezaji wa plastiki na malighafi zingine ni shughuli muhimu nchini Tanzania kwani inasaidia katika kutunza mazingira na kukuza uchumi.

“Tunawaomba UNEP mshirikiane pamoja na Serikali yetu ya Tanzania katika kusaidia kuhakikisha tunakabiliana na kuziondosha kabisa taka za plastiki kwa kuwa na mifumo thabiti ya urejelezaji,” alisema.

Kwa upande wake Bi. Mirey aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake na shirika hilo hususan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya hifadhi ya mazingira.

Alitolea mfano Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi katika Mazingira ya Mkoa wa Kigoma unaofadhiliwa na UNEP kupitia Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) unaoratibiwa chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC).

Bi. Mirey alisema kuwa shirika litaendelea kufadhili mradi huo kupitia mradi huo ambao unaoelenga kuzisaidia jamii zinazozunguka kambi za wakimbizi katika kuhakikisha misitu inarejea.

Pia, alizungumzia mradi wa Bonde la Ziwa Victoria unaolenga kusaidia jamii inayozunguka wenye thamani ya dola milioni 100 sanjari na kuunga mkono miradi ya upandaji

#Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii