Ufaransa kuwaondoa wafanyakazi wake Mali

Duru kutoka wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema nchi hiyo imeanza kupunguza wafanyakazi wake wa kidiplomasia nchini Mali kutokana na hali mbaya ya usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Duru hiyo imesema kwa sasa Ufaransa inafuatilia hali kwa karibu katika taifa hilo. Marekani na Uingereza tayari wamewaondoa wafanyakazi wake huko.

Mali,kama majirani zake katika Ukanda wa Sahel, Burkina Faso na Niger, inatawaliwa kijeshi baada ya mapinduzi na kujitenga na mkoloni wao wa zamani Ufaransa na kujisogeza karibu na Urusi ambayo imewatuma mamluki wake kuwasaidia kupambana na uasi.

Mapema mwezi Septemba, wanamgambo wa Jama'at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM)walitangaza kuzuia uagizaji wa mafuta katika nchi hiyo isiyo na bandari, na tangu wakati huo wamekuwa wakishambulia misafara ya malori ya mafuta yanayojaribu kuingia nchini humo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii