Bunge lajadili tuhuma za mateso ya kidini zinazotuhumiwa kutekelezwa na Nigeria

Bunge la Marekani mnamo Novemba 20 limeijadili Nigeria. Wiki tatu zilizopita, Donald Trump aliitaja Nigeria kama nchi "inayotia wasiwasi kuhusu uhuru wa kidini." Ikulu ya White House inadai kwamba jamii za Kikristo nchini Nigeria zinakabiliwa na mateso makubwa. Wabunge wa Marekani wamejadili kuhusu uungwaji mkono kwa uamuzi wa rais Trump. Wametoa wito wa vikwazo, huku kukiwa na mgawanyiko dhahiri kati ya Wademocrats na Warepublicans.

Wa kwanza kuzungumza alikuwa Mrepublican Christopher Smith, mkongwe wa Kamati ya Mambo ya Nje, ambaye anaunga mkono kikamilifu msimamo wa Donald Trump, anaripoti mwandishi wetu huko Washington, Vincent Souriau. "Nigeria ndiyo kitovu cha mateso makali na hatari zaidi dhidi ya Wakristo ambayo dunia inapitia leo. Serikali ya Nigeria ina wajibu wa kikatiba wa kuwalinda raia wake." Na bado, jambo linalohuunisha ni kwamba wahusika wa uhalifu huu hutekeleza maovu yao bila kuadhibiwa kabisa. Ni maisha ya wakulima Wakristo na familia zao yanayotolewa kafara.

Anatoa wito wa vikwazo kwa watu husika, marufuku ya usafiri, na kuzuiwa kwa mali dhidi ya makampuni na watu binafsi waliohusika na vitendo hivi, huku upande mwingine, Mdemokrasia Sara Jacobs akitoa nafas ya diplomasia ili kuishawishi mamlaka ya Nigeria kuchukua hatua. "Vitisho vya Donald Trump haviwajibiki. Tunahitaji kushirikiana na Nigeria ili kujua jinsi tunavyoweza kuwasaidia kushughulikia jambo hili na kushinikiza mageuzi makubwa ndani ya taasisi za Nigeria."

Bado hakujakuwa na azimio la lazima

Katika hatua hii, hakujakuwa na kura, hakujakuwa na azimio la lazima. Utawala wa Trump umetangaza kwamba ujumbe wa ngazi ya juu wa Nigeria uko Washington wiki hii kujadili suala hilo. Mwanzoni mwa mwez Novemba, rais wa Marekani alitishia Nigeria kuingilia kijeshi kutokana na madai kwamba Wakristo wa nchi hiyo wanauawa. Madai yalikanushwa vikali na Abuja.

Uamuzi wa kuiweka Nigeria kwenye orodha hii ya nchi zenye wasiwasi mkubwa ulifanywa baada ya miezi kadhaa ya ushawishi na wabunge wa kihafidhina wa Marekani, ambao wanaamini kwamba Wakristo nchini humo wanafanyiwa "mauaji ya kimbari." Haya ndiyo maneno yaliyotumika. Mashtaka yanarudiwa na mashirika ya Kikristo na ya kiinjili.

"Ukosefu wa usalama unaua zaidi ya migogoro ya kidini" Azimio la Donald Trump lilipendekeza hasa kutoa msaada wa kibinadamu kwa mashirika ya kidini ambayo husaidia watu waliokimbia makazi yao na kuweka misaada ya Marekani katika hatua madhubuti za serikali ya Nigeria ili kulinda uhuru wa kidini.

Kulingana na viongozi wa kisiasa na watafiti wa Nigeria, ukosefu wa usalama nchini Nigeria unatokana zaidi na ujambazi na migogoro ya rasilimali kuliko migogoro ya kidini. Na kitakwimu, wanajihadi nchini Nigeria wanaua "Waislamu wengi zaidi kuliko Wakristo."

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii