Rais Samia aagiza kuchunguzwa kwa taarifa za waandamanaji kulipwa fedha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati wa Uchaguzi Mkuu kuchunguza kwa kina taarifa za madai ya waandamanaji kulipwa fedha ili kuingia barabarani, pamoja na kubaini chanzo cha fedha hizo na namna zilivyowafikia wahusika.

Akizungumza leo Ikulu Chamwino jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Tume hiyo, Rais Samia ameielekeza Tume kufuatilia ukweli wa madai hayo na kujua fedha hizo zilitoka wapi, ni kina nani waliwapa waandamanaji na ziliwafikaje kwa vijana waliodaiwa kuchochea vurugu.

“Kuna madai kuwa baadhi ya vijana na makundi ya kisiasa walilipwa ili kuchochea hali ile, fedha hizo zilitoka wapi, ziliingia vipi katika mikono ya wanufaika, na Serikali inaweza vipi kudhibiti mazingira ya namna hiyo?” alihoji Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameielekeza Tume kuchambua madai ya msingi ya waandamanaji, ikiwemo kutathmini sababu zilizowafanya vijana waandamane, walikuwa wanadai nini na kipi kinapaswa kufanyike ili kuimarisha amani na haki katika chaguzi zijazo.

#Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii