Ukarabati wa Reli ya TAZARA Dkt. Nchimbi Aiwakilisha Tanzania Katika Uwekaji Jiwe la Msingi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Jijini Lusaka nchini Zambia Novemba 19 mwaka huu kwaajili ya  kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Ukarabati Mkubwa wa Reli ya TAZARA utakaofanyika leo   Novemba 20 mwaka huu Jijini Lusaka.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Makamu wa Rais amepokelewa na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Zambia  Dkt. Elijah Muchima, Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, Maafisa waandamizi wa Jamhuri ya Zambia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoandaliwa kwa heshima yake.

Hata hivyo  Dkt. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja pamoja Mkurugenzi Mkuu TASAC Bw. Mohamed Salum.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii