Wasaidizi 9 wa aliyekuwa Mke wa Rais wa Gabon Wahukumiwa Kwa makosa ya utakatishaji fedha za umma

Mahakama nchini Gabon imewahukumu wasaidizi tisa wa aliyekuwa Mke wa Rais wa Gabon, Sylvia Bongo, na mwanawe Noureddin Bongo, kifungo cha kati ya miaka miwili hadi kumi na tano jela kwa makosa ya utakatishaji fedha na rushwa.

Hukumu hii imekuja siku chache baada ya Sylvia na Noureddin wenyewe kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela bila kuwepo mahakamani.

Aidha kikundi hicho, ambacho kilikuwa kikijulikana kama “Timu ya Vijana,” kiliamriwa pia kulipa kiwango kikubwa cha fidia kinachofikia mabilioni kutokana na uharibifu wa mali ya umma.

Hivyo wasaidizi hao walikamatwa wakati wa mapinduzi ya mwaka 2023, yaliyomuondoa madarakani Rais wa muda mrefu Ali Bongo, aliyekuwa ametawala Gabon kwa miaka 14.

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, mtandao huo ulihusika katika mpango mkubwa wa kufuja fedha za serikali, ambapo walidaiwa kubadilisha na kuhamisha mabilioni ya fedha za umma kwa manufaa binafsi. Fedha hizo zilidaiwa kutumika kununua maeneo ya mafutandege mbili aina ya Boeing, pamoja na mali za kifahari katika Gabon, Morocco na London.

Kiwango cha ufujaji kinakadiriwa kufikia Dola Bilioni 8.6 sawa na takribani Trilioni 20.8 za Kitanzania kikionekana kuwa moja ya kashfa kubwa zaidi za kifedha kuwahi kuripotiwa nchini humo.

Hata hivyo hukumu hizo zinatajwa kuwa sehemu ya juhudi za serikali mpya ya kijeshi kurejesha uwajibikaji, kudhibiti ufisadi na kurudisha mali za umma zilizopotea katika utawala wa Bongo.

#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii