Baraza la Katiba limetangaza tarehe hiyo baada ya kupitia na kukataa rufaa zote zinazohusiana na uchaguzi wa Oktoba 12. Kwa upande wake, Issa Tchiroma Bakary, mgombea urais wa chama cha FSNC anayedai ushindi, amerusha video mpya kutoka mji alikozaliwa wa Garoua, kaskazini mwa nchi. Katika ujumbe huu, anatoa wito kwa wafuasi wake kuendelea kuandamana.
Kinyume na taarifa zinazosambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa siku kadhaa, kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais hakutafanyika leo Alhamisi, Oktoba 23 nchini Cameroon, lakini siku nne baadaye, Jumatatu, Oktoba 27. Tarehe hiyo imetagazwa siku ya Jumatano na Baraza la Katiba, tarehe hii ndiyo pekee itakayozingatiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya taasisi hiyo, ambavyo vinakanusha kuwahi kwa njia yoyote ile, kutaja tarehe ya Oktoba 23...
Tangazo hilo lilitolewa kufuatia kusikilizwa kwa kesi ya rufaa ya uchaguzi wa tarehe 12 Oktoba. Wagombea wanane kwa idadi, karibu wote walitoa wito wa kubatilishwa kwa uchaguzi wa urais kutokana na "udanganyifu mkubwa." Walio wengi walikataliwa kwa sababu za kiutaratibu, kwa kuwa walalamikaji waliokuwa wamewasilisha maombi hayo walikuwa wamewasilisha nje ya muda uliowekwa au hawakuwa na msimamo unaotakiwa wa kukata rufaa kwenye Baraza la Katiba.
Ombi pekee lililochunguzwa kwa kuzingatia sifa, lile la Tomaïno Ndam Njoya, mgombea wa Muungano wa Kidemokrasia wa Cameroon (UDC), pia lilikataliwa. Licha ya maelezo yake marefu na Baraza kuhusu udanganyifu na ukiukaji wa kanuni za uchaguzi ambao yeye na timu zake walibaini wakati wa mchakato wa upigaji kura, chombo hicho kilitangaza kuwa ombi lake halikubaliki baada ya vyama vingine vilivyohusika-ikiwa ni pamoja na mawakili wa Cameroon People's Democratic Movement (CPDM, chama tawala) na Elecam, shirika linalohusika na uchaguzi kwa madai kwamba hawakuunga mkono ushahidi huo.
Kwa upande wa wagombea wa chama cha Social Democratic Front (SDF), Joshua Osih, na chama cha Cameroon Party for National Reconciliation (PCRN), Cabral Libii, ambao pia waliwasilisha maombi ya kubatilishwa kwa sehemu ya uchaguzi, hatimaye waliyaondoa kwa sababu ambazo bado hazijajulikana katika hatua hii.
Wakati wa siku hiyo hiyo ya Jumatano, mgombea wa chama cha National Salvation Front (CNSF), ambaye bado anadai kushinda uchaguzi wa urais, amerusha video mpya kutoka Garoua, mji alikozaliwa kaskazini mwa nchi, ambapo aliwaahidi wafuasi wake kwamba ushindi wao hautaibiwa. Katika taarifa hii iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook, Issa Tchiroma Bakary amedai kuwa alishinda uchaguzi kwa "kiwango cha kihistoria" kabla ya kutoa wito kwa wafuasi wake kuendelea kuandamana kwa amani kutetea chaguo lao. "Ninawaalika Wacameroon wote kutoka kaskazini hadi kusini, kutoka mashariki hadi magharibi, na popote mnapoishi duniani, kujitokeza kama kitu kimoja, kwa amani na kwa upendo wa nchi ya baba. Hebu tuandamane kwa ajili ya ukombozi na kurudisha ushindi wetu," amesema.
Inachukuliwa kuwa "sio tukio" na Wizara ya Mawasiliano, taarifa hii pia imeonekana kuwa ya haraka na Grégoire Owona, Waziri wa Kazi na Naibu Katibu Mkuu wa CPDM, kulingana na madai kwamba Issa Tchiroma Bakary alikosa ushahidi wa kutosha kuunga mkono madai yake. "Nina ... nina hisia kwamba Tchiroma anachukua uchaguzi wa urais kwa mzaha. Hakuweza kutoa ushahidi kwa Tume Kuu au kamati ya madai. Ninamkumbusha kwamba ni vyombo hivi ambavyo huamua nini kitatokea katika uchaguzi wa rais," amesema.