Brigadia Jenerali Ngoy Wa Kabila John akamatwa

Wakili Mkuu Mteule katika Mahakama Kuu ya Kijeshi baada ya kuwa karibu na rais wa sasa wa Kongo, afisa huyu wa zamani wa Joseph Kabila alikamatwa nyumbani kwake Kinshasa usiku wa Jumanne, Oktoba 22 kuamkia Jumatano, Oktoba 23. Taarifa chache zinapatikana katika hatua hii kuhusiana na mazingira au sababu za kukamatwa kwake.

Brigedia Jenerali Ngoy Wa Kabila John alikamatwa mjini Kinshasa. Kulingana na wanafamilia yake, afisa huyu wa zamani wa Joseph Kabila, rais wa zamani wa Kongo aliyehukumiwa kifo kwa "uhalifu wa kivita" na "uhaini" nchini DRC, alikamatwa usiku wa Jumanne, Oktoba 22 kuamkia Jumatano, Oktoba 23.

Karibu saa 7:00 usiku, watu wenye silaha wanaodai kuwa maafisa wa Baraza la Usalama la Kitaifa (CNS) walikwenda nyumbani kwake. Kama vyanzo kadhaa vinadai kuwa hakunyanyaswa, simu zake zilikamatwa. Tangu kukamatwa kwake, Ngoy Wa Kabila John—ambaye baadhi ya washirika wake wa karibu wanasema aliamini kuwa alikuwa akifuatwa kwa siku kadhaa—hajasikika.

Hali ya mashaka

Aliyeteuliwa kuwa Wakili Mkuu katika Mahakama Kuu ya Kijeshi na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi, alikuwa miongoni mwa waliokuwa washirika wa karibu wa mtangulizi wake walioitwa "wasaliti" na kambi yao kwa kujisogeza karibu na utawala wa sasa.

Hii pia ni kesi, kwa mfano, ya Jenerali Pierre Banywesize. Akiwa bado kizuizini kufuatia kukamatwa kwake katika mji mkuu, Kishansa, mnamo mwezi Mei mwaka jana, mkuu huyu wa zamani wa kikosi cha walinzi cha Joseph Kabila amekuwa akihudumu kama naibu kamanda wa kanda ya uendeshaji ya Haut-Uélé kaskazini mwa nchi tangu kuachana na rais wa zamani.

Wakati hali ya mashaka tayari ilikuwapo ndani ya vyombo vya usalama - haswa kati ya maafisa waliofanya kazi na Joseph Kabila - ilichochewa tena katika siku za hivi karibuni na mkutano wa wapinzani kadhaa wa Félix Tshisekedi karibu na Joseph Kabila huko Nairobi, Kenya, Oktoba 14 na 15. Tangu wakati huo, vyombo vya usalama vimekuwa vikitafuta kutambua mawasiliano ya mkuu wa zamani katika serikali na ndani jeshi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii