Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Oktoba 26 mwaka huu aliwasili Seychelles kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais mteule wa sita wa nchi hiyo Dr. Patrick Herminie.
Tume ya Uchaguzi ya Taifa ilimtangaza Mheshimiwa Dkt. Patrick Herminie wa Chama cha United Seychelles (US) kuwa mshindi baada ya kumbwaga Rais aliyekuwa madarakani, Mheshimiwa Wavel Ramkalawan wa Chama cha Linyon Demokratik Seselwa (LDS).
Aidha Dkt. Patrick Herminie alipata asilimia 52.7% ya kura, huku Rais Wavel Ramkalawan akimaliza wa pili kwa kupata 47.3% ya kura.