HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda na Mkandarasi M/s Chonqing International Construction Corporation (CICO), wametiliana saini mkataba wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa Kilomita 8.4.
Makubaliano hayo ya mradi huo wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC), yanajumuisha ujenzi wa barabara 10 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa jengo la usimamizi wa mradi na magari manne ya kusimamia utekelezaji wa mradi.
Makubaliano hayo yamefikiwa leo Oktoba 25 mwaka huu katika halfa iliyofanyika mjini Mpanda mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko.
Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mratibu Msaidizi wa Mradi wa TACTIC, Mhandisi Emmanuel Manyanga, amesema mradi huo utatekelezwa kwa miezi 15 kuanzia Novemba Mosi mwaka huu.
“Ujenzi wa miundombinu hii utahusisha barabara za Mkumbo Junction – Nsemulwa Health Center (Km 1.68), Nsemulwa Health Center – Sokoine (Km 1.23) Kapufi (Mita 760, Sumry (Mita 460), Pinda (Mita 260) Fimbo ya Mnyonge (Mita 390) Fish Market (Mita 330), Mpanda Hotel (Mita 760), Mikocheni Junction – White Gireffe (Km 1.88) na Homeground (Mita 730),” amesema Manyanga.
Mhandisi Manyanga amesema mradi huo utasimamiwa na Mshauri Elekezi M/s NIB Plan Consult