Wasimamizi wa uchaguzi mkuu 2025 wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata Miongozo kanuni na Sheria za uchaguzi pia Kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa kujiamini kwani Jeshi la Polisi Tanzania limewahakikisha ulinzi na usalama wakati wote watakapo kuwa wakitekeleza majukumu yeo.
Wito huo umetolewa na Mrakibu wa Polisi Ahmed Feruzi ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Tarime Oktoba 26 mwaka huu wakati akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tarime Mji katika Ukumbi wa Sekondari ya Tarime Rorya iliyopo MMkoni Mara.
Aidha Feruzi amewataka Wasimamizi hao kuwa mabalozi wazuri wa Amani na kuwataka kuilinda Amani ya nchi kwa maendeleo na ustawi wa taifa kwani Madhara ya Uvunjifu wa Amani ni makubwa na yanayoweza kupelekea kuzorota kwa uchumi, familia kusambaratika na wananchi kushindwa kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii.