Benki ya dunia yaonya mgogoro wa madeni kwa nchi zinazoendelea

Ripoti mpya ya Benki ya dunia inasema baadhi ya nchi maskini zaidi duniani zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni ambao unatatatiza juhudi za kujikwamua kutokana na mdororo wa uchumi uliosababishwa na janga la COVID-19. Zaidi ya nchi 70 za kipato cha chini zinakabiliwa na ulipaji wa madeni ya ziada ya karibu euro bilioni 9.7 mwaka huu ikiwa no ongezeko la asilimia 45 kutoka mwaka uliopita. Ongezeko hilo limetokana na kasi ya ukopaji. Rais wa benki ya dunia David Malpass amesema hali mbaya ya kifedha duniani na masoko duni ya deni la ndani katika nchi nyingi zinazoendelea yanazuia uwekezaji wa kibinafsi na kudhoofisha ufufuaji uchumi. Ripoti hiyo imegusia kukosekana kwa uwazi katika mikopo isiyolipika kuwa kunaathiri upatikanaji wa mikopo kwa kaya za kipato ya chini na biashara ndogo ndogo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii