Wataalamu wa Uturuki waenda Gaza kusaidia kutafuta miili

Uturuki imewatuma wataalamu kadhaa wa uokozi kwenda Ukanda wa Gaza kulisaidia kundi la Hamas kuitafuta miili ya mateka wa Israel ambao inaaminika imefunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoshwa kwa vita.

Tangazo la kutumwa waatalamu hao limetolewa katika wakati hasira inaongezeka nchini Israel hususani miongoni mwa familia za mateka baada ya Hamas kusema imeshindwa kuipata miili ya ndugu na jamaa zao.

Familia hizo zimeitaka serikali ya Israel kusitisha utekelezaji wa hatua zinazofuata za mkataba wa kusitisha vita hadi pale Hamas itakapoikabidhi miili ya mateka 19 waliopoteza maisha wakiwa kizuizini.

Hamas imesema imedhamiria kutimiza matakwa ya mkataba uliosimamiwa na Marekani ikiwa ni pamoja na kuikabidhi miili yote ya mateka itakapopatikana.

Viongozi wa Israel wametishia kuanzisha tena vita au kuzuia upelekwaji misaada Ukanda wa Gaza iwapo miili hiyo haitopatikana haraka.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii