John Bolton, mshauri wa usalama wa kitaifa wa Donald Trump, akabiliwa na mashtaka 18

Aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa wa Donald Trump anakabiliwa na mashtaka 18 yanayohusiana na kumiliki na kufichua nyaraka za siri wakati wa muhula wake wa kwanza. John Bolton, ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa rais, anatuhumiwa kukiuka sheria za ujasusi kama sehemu ya uchunguzi wa mahakama. Katika muda wa mwezi mmoja, nakuwa mkosoaji wa tatu wa wazi wa rais wa Marekani kukabiliwa na kesi za kisheria.

Kulingana na upande wa mashtaka, kati ya mwezi Aprili 2018 na mwezi Agosti 2025, John Bolton alishiriki zaidi ya hati elfu moja: nakala za ratiba yake na maelezo ya shughuli zake rasmi, ikiwa ni pamoja na maelezo yaliyoainishwa kama "siri kuu." Hii ilijumuisha washiriki wawili wa familia yake ambao hawakuidhinishwa kuitazama, anaripoti mwandishi wetu wa Washington, Vincent Souriau.

Kulingana na CNN, watu hawa ni mkewe na binti yake, ambao aliwasiliana nao kupitia barua pepe kutoka kwa ukurasa wa kibinafsi. Jambo linalochukiza ni kwamba ukurasa huu ulidukuliwa baadaye. John Bolton aliarifu serikali, lakini hakuwahi kutaja kuwa ameitumia kuhifadhi habari nyeti.

Nakala zilizochapishwa za kalenda yake pia zilipatikana kutoka nyumbani kwake karibu na Washington wakati wa FBI ikifanya ukaguzi, pamoja na vijitabu kadhaa vilivyotajwa kuwa "siri," au kuainishwa. Aina hii ya fasihi, kwa nadharia, haina sababu ya kuacha majengo rasmi. Ikiwa atapatikana na hatia, John Bolton anakabiliwa na kifungo cha muda mrefu sana jela.

"Mtu mbaya," anashutumu Donald Trump

"John Bolton ni mtu mbaya, ni aibu." "Lakini hivyo ndivyo ilivyo," rais Donald Trump amejibu alipoulizwa kuhusu mashitaka yanayomkaili mshauri wak wa zamani na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House. Donald Trump alielezea mara kwa mara wakati wa kampeni ya uchaguzi nia yake, mara baada ya kurejea madarakani, kulipiza kisasi kwa wale wote anaowaona kuwa maadui wa kibinafsi.

Mashtaka ya John Bolton yanafuatia yale ya aliyekuwa Mkurugenzi wa FBI James Comey na Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la New York Letitia James.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii