Inter Milan yavutiwa na beki wa Palace Marc Guehi

Klabu ya Italia Inter Milan imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Crystal Palace Marc Guehi lakini Liverpool bado wanapewa nafasi kubwa ya kuinasa saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25. (Tuttosport - In Itali)
Mshambulizi wa Bournemouth Antoine Semenyo ana kipengele cha kuachiliwa huru katika kandarasi yake lakini Cherries wanaficha hilo kwa sababu wanataka kusalia na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 25 ambaye amekuwa akihusishwa na Tottenham na Manchester United. (Sportsport)
Chelsea na Barcelona wanamfuatilia mshambuliaji wa Dinamo Zagreb Mreno Cardoso Varela, 16. (Mundo Deportivo - In Spanish)

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii