Simba SC kucheza bila mashabiki na kutozwa faini ya milioni 200

Klabu ya Simba SC haitaruhusiwa kuwa na mashabiki kwenye mchezo wake wa pili dhidi ya Gaborone United baada ya CAF kukataa rufaa yao ya kupinga adhabu ya kucheza bila mashabiki.

Mbali na hilo, Simba imepigwa faini ya jumla ya Dola 85,000 (zaidi ya *Shilingi Milioni 200) kwa makosa yafuatayo: 

- Dola 50,000: Kwa vurugu za mashabiki dhidi ya Al Masry 

- Dola 35,000: Kwa kuwasha fireworks kwenye mchezo dhidi ya RS Berkane

Adhabu hizi zimetolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa mujibu wa kanuni za nidhamu na usalama katika mechi za kimataifa.

Hasara ya kwanza tunakosa mashabiki, hasara ya pili tunakosa mapato na hasara ya tatu tunalipa faini ya USD 50,000. Vilevile tumepewa adhabu kutokana na mechi ya fainaili dhidi ya RS Berkane, huku vilevile tuliwasha fireworks. Kwenye mechi ya fainali tumetozwa faini ya USD 35,000. Jumla Tumetoshwa USD 85,000 sawa na Tsh. 200 milioni.”

“Tunacheza bila mashabiki kwenye mechi dhidi ya Gaborone United pekee lakini sbaabu tumefanya makosa mfululizo CAF watakuwa makini na sisi kwelikweli sababu wanaona tunafanya vitendo ambavyo sio vya kiungwana hivyo watakuwa wanaangalia kama Simba Sports Club tumebadilika. Ni lazima tuwe makini kwelikweli ili kuwaonyesha kwamba tumejifunza na tumebadilika. Kuanzia hivi sasa tuchukue taswira mpya kwenye eneo la ushabiki.”

“Wapo mashabiki ambao wametaka kuwa sehemu ya maumivu ambayo tunapitia Klabu ya Simba na maumivu yenyewe ni faini ya Tsh. 212,500,000 sawa na USD 85,000. Kwa mapenzi yao mashabiki wameomba kuchangia faini ili kuipunguzia klabu mzigo na sisi tumepokea na tumeridhia mashabiki wachangie hususani kwenye eneo la faini.”- Semaji Ahmed Ally.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii