YAS WAIPAMBA LAKE VICTORIA MARATHON MSIMU WA 5

Kama wasemavyo kila hatua mixx  ndivyo mtandao unaoongoza Tanzania nzima kwa 4G na 5G iliyoenea kila kona wamefanikiwa kuigusa kila hatua ya mshiriki katika mbio za kilometa 21,10,5 na 2.5 ndani ya jiji la Mwanza.

Licha ya marathoni hii kuwa na ushindani kwa washiriki bali pia imekuwa chachu ya kuigusa jamii moja kwa moja kwa kukusanya fedha kwaajili ya kutoa msaada kwa Watoto njiti ambao wanauhitaji wa kiungalizi wa hali ya juu.


Lake Victoria marathon imeonyesha wazi kuwa kukimbia si afya pekee bali hata kuigusa jamii inayokuzunguka ni jambo la kupendeza na kuleta tabasamu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii