Yanga Sc leo kibarua wanacho dhidi ya Wiliete FC

Kipyenga cha mashindano ya ngazi ya klabu barani Afrika kimepulizwa wiki hii na leo ni zamu ya mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, ambao watashuka dimbani kuanza safari yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga itashuka dimbani leo Ijumaa Septemba 19 mwaka huu dhidi ya wenyeji wao Wiliete katika mchezo wa hatua ya awali utakaopigwa kwenye Uwanja wa 11 de Novembro uliopo Talatona jijini Luanda kuanzia saa 12:00 jioni kwa saa za Tanzania.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii