Kampuni ya Kitanzania ya JUSTFIT ( @justfitsportsgear ) inayojihusisha na uuzaji na utengenezaji wa vifaa vya michezo Septemba 22 mwaka huu kwa kushirikiana na Bodi ya Ligu Kuu Tanzania, imezindua mpira wa kwanza wa Ligi kuu ambao ni mpira rasmi utakaokuwa ukitumika katika msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara.
Mbali na mpira huo, JUSTFIT ambao wanamiliki Maduka mbalimbali yanayouza vifaa vya michezo na mazoezi, pia wametengeneza jezi za Marefa ambazo zitavaliwa katika kipindi chote cha Msimu wa Ligi kuu Tanzania bara.
Mpira huu ni ubunifu wa Kitanzania ambao umebeba alama ya ubunifu, upekee na ubora wa hali ya juu kwa viwango vya kidunia ambapo uzinduzi wake umehudhuriwa na Salim Salim ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JUSTFIT akiwa na Makamu wa Rais wa TFF Athuman Nyamlani na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu Ibrahim Mwayela.