Klabu ya Chelsea imefufua tena azma ya kumsajili kipa wa Ufaransa na AC Milan Mike Maignan, 30, na huenda ikamjumuisha kwenye orodha ya uhamisho katika dirisha lijalo la usajili wa wachezaji baada ya kipa wake wa sasa Mhispania Robert Sanchez, 27, kutofanya vizuri katika mechi yao dhidi ya Manchester United siku ya Jumamosi. (Daily Express)
Mkufunzi wa Brighton Fabian Hurzeler amemtaka kiungo Carlos Baleba kusalia licha ya tetesi kuibuka kwamba anandoka, huku Manchester United ikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21 msimu wa kiangaza. (Daily Mirror)
Everton wanafikiria kumsajili mchezaji huru Sergio Reguilon, 28, lakini beki huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur anasemekana kupendelea kurejea katika nchi yake ya Uhispania. (Football Insider)