Watu zaidi ya 800 wamefariki na wengine zaidi ya 2,700 wamejeruhiwa mashariki mwa Afghanistan, ambayo imekumbwa usiku na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6 lenye ukubwa wa 6 katika kipimo cha Richter, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Abdul Mateen Qani ameliambia shirika lahabari la AFP leo Jumatatu, Septemba 1.
Kitovu cha tetemeko la ardhi, umbali wa kilomita nane tu, kimepatikana kilomita 27 kutoka Jalalabad, mji mkuu wa mkoa wa Nangarhar, kwenye mpaka na mkoa jirani wa Kunar, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.
Idadi ya vifo ni kubwa zaidi katika mkoa huu wa mwisho, na ni katika eneo hili ambapo helikopta za uokoaji zinazotumwa na mamlaka ya Taliban zinaelekea Jumatatu asubuhi. Tangu kurejea kwao madarakani mwaka 2021, tayari wamekumbana na tetemeko jingine kubwa la ardhi: mwaka 2023, huko Herat, upande wa pili wa nchi, magharibi mwa mpaka wa Iran, zaidi ya watu 1,500 walifariki na zaidi ya nyumba 63,000 ziliharibiwa.
Wakati huu, idadi ya vifo vya muda inaonyesha "watu 610 wamekufa na 1,300 kujeruhiwa katika mkoa wa Kunar, pamoja na 12 waliofariki na 255 kujeruhiwa katika mkoa wa Nangarhar," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani huko Kabul, Abdul Mateen Qani, ameliambia shirika la habari la AFP.
Maafisa wa Afghanistan, ambao mara kwa mara wanasisitiza kwamba idadi ya vifo itabadilika huku utafutaji wa watyu waliokwama chini ya vifusi na manusura ukiendelea katika maeneo haya ya mbali na machafu, wanasema uharibifu ni "mkubwa sana" huko Kunar.
Afghanistan hukumbwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara, haswa katika safu ya milima ya Hindu Kush, karibu na makutano ya miamba ya Eurasia na India. Lakini yale yliyotokea katikati ya usiku—na kufuatiwa na mitetemeko mitano ya baadaye, ikiwa ni pamoja na ile yenye ukubwa wa 5.2—ilikuwa mikubwa hasa. Waandishi wa habari wa AFP wamehisi mitetemeko huko Kabul kwa sekunde kadhaa, na vile vile huko Islamabad, Pakistan, umbali wa kilomita 370.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, mojawapo ya vituo vya mwisho vya usalama katika nchi ambayo imebeba mzigo mkubwa wa kupunguzwa kwa misaada ya kibinadamu ya kimataifa hivi karibuni, umesema "umehuzunishwa sana na tetemeko la ardhi ambalo limesababisha vifo vya mamia ya watu." "Timu zetu ziko uwanjani kutoa usaidizi wa dharura," umeongeza.
Mkoa wa Nangarhar tayari ulikumbwa na mafuriko wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu watano na kusababisha uharibifu mkubwa, wa mashamba na makazi. Mnamo mwezi Oktoba 2023, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 katika kipimo cha Richter huko Herat, likifuatiwa na mitetemeko minane ya baadaye, lilikuwa tetemeko baya zaidi kuwahi kuikumba nchi hii, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, katika zaidi ya miaka 25. Kulingana na Benki ya Dunia, karibu nusu ya wakazi wa Afghanistan wanaishi katika umaskini.