Tamasha jipya la muziki na utamaduni, Futopia Festival 2025, limeendelea kuteka hisia za mashabiki waliomiminika Fumba Town, Zanzibar. Baada ya siku ya kwanza iliyojaa surprises, Day 2 ilizidi kuonyesha ukubwa na upekee wa Futopia midundo, furaha na vibes kali zisizo na mfano.
Bensoul (Kenya): Soul na Vibe ya Tanzania
Kutoka Kenya, Bensoul alikuja na Afro-Soul yenye roho na mashairi yanayogusa. Zaidi ya performance yake kali, alisisitiza namna anavyopenda vibe ya Tanzania na jinsi mashabiki walivyomkaribisha kwa upendo mkubwa. Bensoul hakuficha furaha yake akasema wazi kuwa Tanzania ni moja ya sehemu anazozipenda sana sana sana.
Rosaree alithibitisha tena kuwa Tanzania ina vipaji vinavyoweza kushindana kimataifa. Performance yake ilikuwa na nguvu, confidence na sauti ya kipekee iliyowaweka mashabiki wote macho jukwaani. Kwa Rosaree, Futopia siyo tu show bali ni kitu kikubwa, kipya na cha kipekee ambacho kimempa fahari kushiriki.
Bonj (Afrika Kusini): Sauti Kali, Upendo kwa Singeli
Kutoka Afrika Kusini, Bonj alitoa show yenye hisia, vocal power na charisma ya hali ya juu. Aliwaambia mashabiki jinsi alivyovutiwa na performance za siku ya kwanza, hasa zile kutoka Tanzania. Zaidi ya yote, alifichua kuwa ameupenda sana muziki wa singeli kitu ambacho kilimfanya ahisi vibe ya kipekee ya Futopia.
Mubah (Tanzania): Muziki wa Jazz na Afrobeat Jukwaa Moja
Mubah alikuja na ladha tofauti muziki wa jazz uliyojaa bashasha huku mashabiki wakifurahia utofauti na ubunifu. Show yake ilionyesha upeo wa muziki wa Tanzania unaojengwa kwa mitindo mbalimbali.
Kwa kufunga dimba la siku ya pili, Tribal Native walipiga midundo mizito iliyochanganya tamaduni na muziki wa kisasa. Hadhira ilicheza bila kuchoka, na kwa muda ilihisi kama wote wamesafirishwa kwenye safari ya muziki ndani ya Afrika lakini bado wakihisi nyumbani pale Fumba Town.
Siku ya pili ya Futopia ilikuwa zaidi ya muziki. Ilikuwa ni sherehe ya tamaduni, ushirikiano na ubunifu. Mashabiki walifurahia, walishangilia na walicheza mpaka mwisho wa usiku..
Fumba Town iliwaka moto. Day 3 inabakia kuandika historia zaidi lakini siku ya pili imehakikisha Futopia sio tu tamasha, ni harakati mpya ya muziki wa Afrika.