SAUTI ZA BUSARA 2026: MUZIKI WA KIAFRIKA UKIKUSANYIKA ZANZIBAR

Tamasha la Sauti za Busara 2026 linarudi kwa shauku kubwa kutoka 5–8 Februari katika mji wa kihistoria wa Stone Town, Zanzibar. Tukio hili la mwaka la 23 litasherehekea muziki wa Kiafrika, utamaduni, na ubunifu kupitia maonyesho ya moja kwa moja kutoka kwa wasanii wa ndani na kimataifa.

Mwenye sauti ya kipekee, Salif Keïta, maarufu kama The Golden Voice of Africa, atapamba tamasha na shoo yake ya kipekee, akichanganya miziki ya jadi ya Mandé na sauti za kisasa. Mbali na Keïta, tamasha litakuwa na maonyesho kutoka kwa wasanii kama Ben Pol, Man Fongo, Pilani Bubu, Lindigo, Sousou & Maher Cissoko, Mama C & The Fusion Band, na wengine wengi.


Sauti za Busara ni zaidi ya burudani ni fursa ya kusherehekea utofauti wa kitamaduni, kukuza utalii wa muziki, na kuungana kwa umoja wa Kiafrika chini ya anga la Zanzibar. Kwa wale wanaopenda muziki wa Kiafrika na uzoefu wa tamasha la kipekee, Sauti za Busara 2026 ni tukio lisilosahaulika.

 Jiandae kufurahia Afrika chini ya anga la Afrika!

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii