MSIGWA AWAKABIDHI UMSOTA MILIONI TANO ZAWADI YA “GOLI LA MAMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa amekabidhi kiasi cha shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa timu ya Umoja wa Maveterani wa Soka Tanzania (UMSOTA) kama zawadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amekabidhi fedha hizo Oktoba 23 mwaka huu  jijini Dar es Salaam katika hafla maalum ya kuipongeza timu hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya soka ya Maveterani Afrika Mashariki yaliyofanyika  Oktoba mosi mwaka huu nchini Kenya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UMSOTA Bw. Paul Ambrose Lusozi maarufu kama Father aliishukuru Serikali kwa kutambua mafanikio yao akiahidi kuwa timu hiyo itaendelea kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuimarisha umoja na kukuza michezo miongoni mwa maveterani.

Mashindano hayo ya Afrika Mashariki yalihusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii