Alassane Ouattara ashinda kwa kishindo, kulingana na matokeo ya awali

Alassane Ouattara, ambaye ameiongoza Côte d'Ivoire tangu mwaka 2011, ametangazwa kushinda uchaguzi wa urais wa Oktoba 25, 2025, kwa kishindo, kwa asilimia 89.77 ya kura, kulingana na matokeo ya jumla ya awali yaliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi (IEC) siku ya Jumatatu Oktoba 27. Baraza la Katiba litatangaza matokeo ya mwisho baada ya kipindi cha mizozo ya uchaguzi.

"Alassane Ouattara, asilimia 89.77!" » Na rais wa Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) ametangaza "usindi mkubwa" kwa mkuu wa nchi katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Côte d'Ivoire mnamo mwaka 2025. Ingawa matokeo bado hayajakamilika, kiongozi huyo ambaye ameiongoza Côte d'Ivoire tangu mwaka 2011 anaelekea muhula wa nne akiwa kiongozi wa nchi, kufuatia kuchaguliwa tena mwaka 2015 na 2020. Siku ya Jumatatu, CEI imetangaza kwamba Alassane Ouattara, 83, yuko mbele ya wapinzani wake wanne: Simone Ehivet wa chama cha Movement of Capable Generations (2.42%), Jean-Louis Billon wa chama cha Democratic Congress (3.09%), Ahoua Don Mello, mgombea binafsi (1.97%), na Henriette Lagou wa kundi la vyama vya siasa kwa ajili ya amani (1.15%).

Mapema Jumapili jioni, Jean-Louis Billon "alimpongeza Alassane Ouattara kwa kuchaguliwa tena," huku akisema kwamba "mchakato huo haukuwa huru kutokana na ukiukwaji wa sheria" na kuhtumu "kiwango cha chini ushiriki, haswa katika baadhi ya maeneo."

Anaongoza kwa tofauti kubwa katika majimbo yote

Ikilinganishwa na uchaguzi wa urais uliopita, mwaka wa 2020, Alassane Ouattara alifanya vibaya kidogo (95.31% miaka mitano iliyopita) na bora zaidi kuliko mwaka wa 2015 (83.66%). Alama zake zilikuwa karibu na 100% katika maeneo kadhaa kaskazini mwa nchi, kama vile Kani (99.68% ya kura na 99.08% ya kiwango cha ushiriki). Na aliongoza kwa tofauti kubwa katika kila jimbo (idara, manispaa, na vituo vya kupigia kura vya ng'ambo).

Hata hivyo, kiwango cha waliojitokeza kimeshuka kidogo, kulingana na takwimu hizi rasmi - 50.10% ikilinganishwa na 53.90% mwaka wa 2020 na 52.86% mwaka wa 2015 - wakati mwingine kura za chini sana kulingana na eneo la kijiografia, kama vile katika eneo la Gagnoa (20.68%) au wilaya huko Abidjan kama vile Cocody (19.24%).

Sasa ni wakati wa Baraza la Katiba, jaji pekee wa uchaguzi, na baada ya kipindi cha mizozo ya uchaguzi,kutangaza mgombea rasmi. Ni mwishoni mwa kipindi hiki ambapo mahakama itatangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi huu wa saba wa urais tangu ujio wa siasa za vyama vingi nchini Côte d'Ivoire.

Common Front inadai "uchaguzi mpya na wa kuaminika"

Ingawa uchaguzi wa Jumamosi ulifanyika kwa amani kwa ujumla, ghasia ziliripotiwa katika 2% ya maeneo ya kupigia kura, au takriban maeneo 200, kulingana na ripoti ya vikosi vya usalama iliyotolewa kwa shirika la habari la Agence France-Presse (AFP). Jumla ya watu kumi wamefariki tangu katikati ya mwezi Oktoba kando ya mchakato wa uchaguzi, wakiwemo sita kabla ya uchaguzi, kulingana na Baraza la Kitaifa la Haki za Binadamu (CNDH). Siku ya Jumatatu asubuhi, mgombea Ahoua Don Mello alilaani "ukatili uliofanywa Nahio," katika idara ya Haut-Sassandra (katikati-magharibi), ambapo watu wawili waliuawa. Nchini Côte d'Ivoire, uchaguzi wa urais mara nyingi huonekana kama wakati wa mivutano ambayo inaweza kuzidi kugeuka na kuwa vurugu, hasa kama wakati wa mgogoro wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011, ambao ulisababisha vifo vya takriban watu 3,000.

Viongozi wawili wakuu wa upinzani, Laurent Gbagbo wa Chama cha PPA-CI na Tidjiane Thiam wa chama cha PDCI-RDA, watu wawili mashuhuri ambao hawakushiriki uchaguzi wa urais wa 2025. Wagombea wao walikataliwa na Baraza la Katiba.

Katika taarifa siku ya Jumapili jioni, jukwaa la pamoja la PPA-CI na PDCI-RDA, Common Front, lilidai "linatakakwa kufanyika kwa chaguzi mpya ambazo ni za kuaminika, za uwazi, zinazojumuisha wote, na kwa mujibu wa Katiba," wakishutumu "udanganyifu wa uchaguzi" na "kwenda kinyume na matakwa ya raia."

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii