Msanii Mkongwe wa R&B, D’Angelo Afariki Dunia Akiwa na Miaka 51

Mwanamuziki maarufu wa Marekani, Michael Eugene Archer almaarufu D’Angelo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 51 baada ya kusumbuliwa na saratani ya kongosho kwa muda mrefu.

Mkali huyo wa miondoko ya R&B ambaye anajulikana kwa nyimbo kama ‘Brown Sugar’ na ‘Untitled (How Does It Feel)’ alikuwa mmoja wa waasisi wa muziki wa neo-soul, akichanganya ladha za gospel, funk na R&B kwa namna ya upekee.

D’Angelo alibadilisha kabisa sura ya muziki wa kisasa kupitia albamu zake kama Brown Sugar (1995), Voodoo (2000) iliyompatia tuzo ya Grammy na Black Messiah (2014) akifanya kazi na wakali kama Jay Z, Erykah Badu, Q-Tip, na wengine wengi.

Mashabiki na wasanii wenzake duniani kote wanaomboleza kifo cha cha msanii huyo ambaye ameacha alama kubwa katika ulimwengu wa muziki huku wakimtaja kama mwana-soul halisi aliyeleta uhai mpya kwenye muziki wa R&B.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii