FUTOPIA ZANZIBAR: SIKU YA KWANZA HAIKUPOA

Zanzibar jana ilikuwa sehemu ya moto kabisa baada ya kuzinduliwa rasmi kwa tamasha jipya la Futopia. Siku ya kwanza pekee imeonyesha wazi kuwa hili si tukio la kawaida, bali ni jukwaa jipya la muziki na burudani ambalo limekuja kuandika historia yake.

Kutoka mwanzo mpaka mwisho, mashabiki walipata mchanganyiko wa ladha tofauti tofauti. DJ KMC alianzisha vibe kwa set kali zilizoandaa anga la sherehe, kisha akafuatiwa na Tryphon Evarist kutoka Zanzibar mwenyewe, aliyewasha jukwaa kwa style ya kipekee. Wakati kundi la Warriors from the East walipopanda stejini, mashabiki walihisi nguvu ya muziki wa Tanzania bara ikitikisa ukumbi.


Wamoto band TZ

Lakini burudani haikuishia hapo. Damian Soul alileta ule utulivu wenye vionjo vya soul na Afro-fusion, akawasukuma mashabiki kwenye safari ya muziki iliyojaa hisia. Hatua ya kilele ikafika pale kundi la Wamoto walipochukua usukani  na kweli, jukwaa likawaka moto! Mashabiki waliruka, walipiga kelele, na furaha ilichukua usiku mzima.

Kwa ujumla, siku ya kwanza ya Futopia imeonyesha dira mpya ya burudani ndani ya Zanzibar. Kama hii ndiyo mwanzo, basi kilicho mbele kitakuwa zaidi ya kawaida.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii