KHALID Aucho kiungo wa zamani wa Yanga SC inatajwa kuwa amefikia makubaliano mazuri na Singida Black kuelekea msimu wa 2025/26.
Kiungo huyo ni moja ya wachezaji waliowahi kufundishwa na Miguel Gamondi ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Singida Black Stars.
Anajiunga na Singida Black Stars ambayo inapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo.
Taarifa zinaeleza kuwa Aucho yupo tayari kambini na timu ya Singida Black Stars ambayo kwa sasa ipo Dar kwa maandalizi ya msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na itashiriki Kagame Cup.
Miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajiwa kuwa kwenye kikosi cha Singida Black Stars kwenye mashindano hay oni Aucho ambaye anasajiliwa na timu hiyo akiwa ni mchezaji huru mara baada ya mkataba wake kuisha Yanga SC.