Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya 2025/2026 itachezwa uwanja wa Puskas Arena

Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) imeamua Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2025/2026 itachezwa katika Uwanja wa Puskas Arena, Budapest Hungary.

Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano hayo mechi hiyo ya Fainali itafanyika Jumamosi Mei 30, 2026.

Uwanja huo ndio ulitumika kwa mechi ya Fainali ya Europa League msimu wa 2022/2023 ambayo Sevilla iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 4-1 dhidi ya AS Roma baafa ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Je Unaiona timu yako ikiwa miongoni mwa mbili zitakazocheza fainali hiyo msimu huu?


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii