Fadlu Davids apongeza kiwango cha wachezaji wake

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amepongeza kiwango cha wachezaji wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia katika tamasha la 17 la Simba Day lililofanyika Septemba 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

‎‎Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Fadlu amesema mechi ilikuwa nzuri na imempa fursa ya kuona namna kikosi chake kinavyoanza kuzoea mfumo mpya wa uchezaji.

‎Kocha huyo amefafanua kuwa bado kuna mambo ya kurekebisha, hasa katika kuelewa jinsi ya kucheza na mpira na bila mpira, lakini akaeleza kuridhishwa kwake na hatua za awali.

‎‎"Nimeridhishwa sana na kikosi hiki. Ingawa bado wapo kwenye hatua ya kujifunza maelekezo ya mbinu zetu, naamini kadri muda unavyokwenda tutapata muunganiko mzuri zaidi. Kwa sasa ni hatua ya mwanzo nzuri," aliongeza.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii