Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kongamano la kitaifa la ufuatiliaji, tathmini

 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kitaifa la ufuatiliaji, tathmini na kujifunza, litakalofanyika jijini Mwanza kuanzia kesho Septemba 10 hadi 13 mwaka huu wa Maraika beach jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya mkoa  wa Mwanza , Mtanda amesema kuwa  ufuatiliaji wa kongamano hilo ni silaha muhimu kwa serikali katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati, na ubora wa tathimini halisi  ya fedha kutokana ufuatiliaji wa tathmini unaoendelea kufanyika mara kwa mara jambo lililopelekea kumewezesha utekelezaji wa miradi yenye thamani ya Sh trilioni 5.6 mkoani Mwanza, iliyotolewa na serikali kuu kuanzia mwaka 2021 hadi 2025.

Aidha miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Daraja la JPM lililopo kigongo busisi, meli ya MV Mwanza, vivuko vipya, hospitali ya hadhi ya kutoa huduma za kibingwa wilayani Ukerewe, soko kuu la kisasa pamoja na kipande cha reli ya  kisasa SGR cha Mwanza–Kahama.


Hata hivyo amesema kongamano hilo litakutanisha washiriki 1,000 kutoka ndani na nje ya Tanzania chini ya kauli mbiu isemayo'' Kuimarisha ufuatiliaji na tathimini katika ngazi ya jamii ili kuleta maendeleo endelevu''

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii