Urusi ilirusha makombora na ndege zisizo na rubani 85 kuelekea Ukraine

Urusi ilirusha makombora na ndege 85 zisizo na rubani nchini Ukraine usiku wa kuamkia leo kulingana na taarifa ya Kyiv.

Taarifa ya Kyiv  imejiri saa chache kupita tangu kukamilika kwa kikao kati ya Rais Vladimir Putin na mwenzake wa Marekani Donald Trump jijini Alaska.

Mazungumzo hayo ambayo yalikuwa yametarajiwa pakubwa yalitamatika bila ya kupatikana kwa mwafaka wa kumaliza mapigano ya zaidi ya miaka miwili sasa nchini Ukraine.

Katika ripoti yake ya kila siku, jeshi la anga la Ukraine limethibitisha kutokea kwa mashambulio hayo yalianza usiku wa tarehe 15 hadi usiku wa kuamkia tarehe 16 wakati ambapo Putin na Trump walipokuwa na mazunguzmo.

Awali Kyiv ilikuwa imethibitisha kuangusha ndege 61 zisizokuwa na rubani.

Kikao kati ya Trump-Putin kilitamatika bila ya kupatikana kwa suluhu licha ya miezi kadhaa ya shinikizo kwa Kremlin kutoka kwa nchi za Magharibi kumaliza vita hivyo.

Katika hatua nyengine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kwamba atakutana na mwenzake wa Marekani jijini Washington wiki ijayo.

Urusi ilianzisha uvamizi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka wa 2022, maelfu ya watu wakiwa wameuawa katika uvamizi huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii