Simba Fanyeni Kweli Uwanja wa Mkapa Leo

SIMBA SC, leo Jumapili inatarajiwa kuvaana na ASEC Mimosas katika mchezo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Saalam.

Huu utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba katika hatua hii ikiwa ni timu pekee ya Tanzania katika michuano  hiyo.

Simba imekuwa na historia nzuri katika michuano hiyo ya kimataifa kwa siku za karibuni, tunaamini kuwa wataenda
kufanya kweli kuanzia mchezo
wa leo wakiwa Kundi D.

Tunafahamu huu utakuwa ni mchezo mgumu kwa Simba, lakini wanatakiwa kupambana kwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Simba wanatakiwa kupambana mpaka hatua ya mwisho kwa kuhakikisha wanapata matokeo bora ili kujitengenezea nafasi ya kusonga mbele hatua ya robo fainali.

Wachezaji wanatakiwa kuingia kwa tahadhari kubwa na nidhamu katika mchezo huo kwani wapinzani wao si
timu ya kuibeza.


Tunaamini kuwa Simba watautumia vema uwanja wa nyumbani kwa kupata matokeo mazuri ya ushindi ikiwa ni sehemu ya kujitengenezea mazingira ya kufikia malengo.

Watanzania na mashabiki wa soka wapo nyuma yenu Simba kuhakikisha mnafanikiwa kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.

Hakuna kinachoshindikana. Kila la kheri Simba SC, wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki kwenye
michuano ya Kombe la
Shirikisho Afrika msimu huu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii